4 1 Sam 14:34;Mdo 15:20,29;Law 7:26-27;17:10-14;19:26;Kum 12:16,23;15:23Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. 5 Kut 21:28,29;Hes 35:31;Mdo 17:26Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. 6 Kut 21:12,14;Law 24:17;Mt 26:52;Ufu 13:10;1 Kor 11:7;Mwa 1:26;Kut 20:13Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.