35 Ebr 11:6Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. 36 Ebr 6:12;Lk 21:19Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.
37 Hab 2:3-4;Isa 26:20;Lk 21:28;Yak 5:8Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana,
Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.
38 Rum 1:17;Gal 3:11Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.