Maonyo juu ya kukataa neema ya Mungu
14 Zab 34:14;Mt 5:8;Rum 12:18;2 Tim 2:22Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 Kum 29:18;Mdo 8:23mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.