Publicidade

Hebreus 12

5 Ayu 5:17;Mit 3:11-12tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana,

Mwanangu, usiyadharau maonyo ya Bwana,

Wala usife moyo ukiadhibiwa naye;

6 Ufu 3:19Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humuonya

Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

7 Ni kwa ajili ya kuonywa mnastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyeonywa na babaye? 8 Zab 73:14,15Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Hes 16:22Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-