5 Kum 31:6,8;Yos 1:5;1 Tim 6:6Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha. 6 Zab 118:6Hata tunathubutu kusema,
Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?