Maonyo juu ya uasi
11 Yeye ambaye tuna maneno mengi ya kunena kuhusu habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12 1 Kor 3:2;1 Pet 2:2Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13 Efe 4:14Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14 Flp 1:10;Rum 16:19;Mwa 2:17Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.