Publicidade

Hebreus 5

1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yanayomhusu Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; 2 Ebr 4:15 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe ana udhaifu; 3 Law 9:7;16:6 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. 4 Kut 28:1 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. 5 Zab 2:7;Mdo 13:33 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,

Ndiwe mwanangu,

Mimi leo nimekuzaa.

6 Zab 110:4;Ebr 7:1 Kama asemavyo mahali pengine,

Ndiwe kuhani milele

Kwa mfano wa Melkizedeki.

7 Mt 26:36-46;Mk 14:32-42;Lk 22:39-46 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 8 Flp 2:8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 9 Isa 45:17;Yn 17:1,5 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; 10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Maonyo juu ya uasi

11 Yeye ambaye tuna maneno mengi ya kunena kuhusu habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12 1 Kor 3:2;1 Pet 2:2 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13 Efe 4:14 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14 Flp 1:10;Rum 16:19;Mwa 2:17 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-