23 Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae; 24 bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. 25 Rum 8:34;1 Yoh 2:1Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
26 Ebr 4:14Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; 27 Law 9:7;16:6,15ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.