1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia. 2 Kut 26:1-30;25:23-40Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate mitakatifu; ndipo palipoitwa, Patakatifu. 3 Kut 26:31-33Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu, 4 Kut 16:33;25:10-16,21;30:1-6;Hes 17:8-10;Kum 10:3-5yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; 5 Kut 25:18-22;26:34na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.
Publicidade
Hebreus 9
Maskani ya duniani na ya mbinguni