Publicidade

Habacuque 3

Ombi la nabii

1 Sala ya nabii Habakuki.3:1 iliyoimbwa kwa Shigionothi.

2 Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa;

Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka;

Katikati ya miaka tangaza habari yake;

Katika ghadhabu kumbuka rehema.

3 Mungu alikuja kutoka Temani,

Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani.

Utukufu wake ukazifunika mbingu,

Nayo dunia ikajaa sifa yake.

4 Mwangaza wake ulikuwa kama nuru;

Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake;

Ndipo ulipofichwa uweza wake.

5 Mbele zake ilikwenda tauni,

Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake.

6 Kut 23:31;Kum 32:8;Hes 21:24,34 Akasimama na kuitikisa dunia;

Akatazama, mataifa yakatetemeka;

Na milima ya zamani ikatawanyika;

Vilima vya kale vikainama;

Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.

7 Niliziona hema za Kushani zikitaabika;

Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.

8 Kut 14:21,22 Je! BWANA aliikasirikia mito?

Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito,

Au ghadhabu yako juu ya bahari,

Hata ukapanda farasi wako,

Katika magari yako ya wokovu?

9 Uta wako ukafanywa wazi kabisa;

Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti;

Ukaipasua nchi kwa mito.

10 Milima ilikuona, ikaogopa;

Gharika ya maji ikapita;

Vilindi vikatoa sauti yake,

Vikainua juu mikono yake.

11 Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao;

Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa,

Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.

12 Zab 44:2,3;Mik 4:13 Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu;

Ukawapura mataifa kwa hasira.

13 2 Sam 5:20 Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako,

Kwa ajili ya wokovu wa masihi3:13 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wako;

Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu,

Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.

14 Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe;

Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya;

Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.

15 Ukaikanyaga bahari kwa farasi wako,

Chungu ya maji yenye nguvu.

16 Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka,

Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile;

Ubovu ukaingia mifupani mwangu,

Nikatetemeka katika mahali pangu;

Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki,

Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.

Imani na shangwe katika shida

17 2 Kor 4:8,9 Maana mtini hautachanua maua,

Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda;

Taabu ya mzeituni itakuwa bure,

Na mashamba hayatatoa chakula;

Zizini hamtakuwa na kundi,

Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe;

18 Zab 42:5;Isa 61:10 Walakini nitamfurahia BWANA

Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.

19 2 Sam 22:34;Zab 18:33;27:1 MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu,

Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu,

Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.3:19 Na apewe mwimbishaji mkuu kwa vinanda vyangu vyenye nyuzi.

Veja também

Habacuque
Ver todos os capítulos de Habacuque
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-