12 Yer 4:1;Hos 12:6Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza; 13 2 Fal 22:19;Zab 34:18;Isa 57:15;Mt 5:3,4;Kut 34:6;Yon 4:2rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi kuadhibu. 14 Yos 14:12;Sef 2:3;Isa 65:8;Hag 2:19Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?
15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni,
Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;
16 Kut 19:10;2 Nya 20:13;1 Kor 7:5Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko,
Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto,
Na hao wanyonyao maziwa;
Bwana arusi na atoke chumbani mwake,
Na bibi arusi katika hema yake.
17 Mt 23:35;Kut 32:11;Isa 37:20Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie
Kati ya patakatifu na madhabahu,
Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA,
Wala usiutoe urithi wako upate aibu,
Hata mataifa watawale juu yao;
Kwa nini waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?