Publicidade

Jonas 2

Wimbo wa kushukuru

1 Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, akiwa katika tumbo la yule samaki, 2 Akasema,

Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,

Naye akaniitikia;

Katika tumbo la kuzimu niliomba,

Nawe ukasikia sauti yangu.

3 Zab 88:6 Maana ulinitupa vilindini,

Ndani ya moyo wa bahari;

Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;

Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

4 Zab 31:22;Isa 49:14;1 Fal 8:38 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;

Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;

Vilindi vilinizunguka;

Mwani ulikizinga kichwa changu;

6 Nilishuka hata pande za chini za milima;

Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele;

Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni,

Ee BWANA, Mungu wangu,

7 Zab 18:6;34:6;130:2;Yer 2:13 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,

Nilimkumbuka BWANA;

Maombi yangu yakakufikia,

Katika hekalu lako takatifu.

8 2 Fal 17:15;Zab 31:6;Yer 10:8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo

Hujitenga na rehema zao wenyewe.

9 Zab 50:14;66:13-15;Hos 14:2;Ebr 13:15 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;

Nitaziondoa nadhiri zangu.

Wokovu hutoka kwa BWANA.

10 Yon 1:17;Mt 8:9 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.

Veja também

Jonas
Ver todos os capítulos de Jonas
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-