Pular para o conteúdo
Publicidade

Jonas 3

5 Mt 12:41;Lk 11:32Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, kuanzia yeye aliye mkubwa hadi aliye mdogo. 6 Ayu 2:8;Yer 6:26;Omb 3:29;Mik 1:10Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. 7 2 Nya 20:3;Yoe 2:15Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; 8 Isa 1:16;Eze 33:11;Dan 4:27bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. 9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

Veja também

Jonas
Ver todos os capítulos de Jonas