Neno akawa mwili
1 1 Yoh 1:1,2;Yn 17:5;Ufu 19:13Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Mit 8:22Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Kol 1:16,17;Ebr 1:2Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.