Pular para o conteúdo
Publicidade

João 12

Yesu aingia Yerusalemu kwa ushindi

12 Mt 21:1-11;Mk 11:1-10;Lk 19:29-40Nayo kesho yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; 13 Zab 118:25,26wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! 14 Zek 9:9Naye Yesu alikuwa amepata mwanapunda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, 15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda. 16 Yn 7:39Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo. 17 Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua. 18 Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo. 19 Yn 11:48Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lolote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.

Veja também