Njama za kumwua Lazaro
9 Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu. 10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; 11 maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu.
17 Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua. 18 Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.