Njama ya kumuua Lazaro
9 Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Isa alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Isa, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Isa alikuwa amemfufua. 10 Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakapanga njama ya kumuua Lazaro pia, 11 kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake, Wayahudi wengi walikuwa wanamfuata Isa na kumwamini.
Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe
(Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40)
17 Wale waliokuwepo Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu waliendelea kushuhudia. 18 Na kwa sababu walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu, umati wa watu wakaenda kumlaki.