Pular para o conteúdo
Publicidade

João 15

Yesu ni mzabibu wa kweli

1 Yer 2:21;Zab 80:8Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Mt 15:13Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi hamuwezi, msipokaa ndani yangu. 5 1 Kor 12:12,27;2 Kor 3:5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.

Veja também