Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 19:12-16

SRUV Swahili Revised Union Version

12 Mdo 17:7Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari. 13 Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha. 14 Nayo ilikuwa Maandalio ya Pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! 15 Yn 19:6Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulubishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulubishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.

Kusulubiwa kwa Yesu

16 Mt 27:31-50;Mk 15:20-37;Lk 23:26-46Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulubiwe; nao wakampokea Yesu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Isa, lakini viongozi wa Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, "Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu yeyote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari."

    13 Pilato aliposikia maneno haya, akamtoa Isa nje tena. Akaketi kwenye kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe (kwa Kiebrania ni Gabatha). 14 Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi.

    Pilato akawaambia Wayahudi, "Huyu hapa mfalme wenu!"

    15 Wao wakapiga kelele, "Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!"

    Pilato akawauliza, "Je, nimsulubishe mfalme wenu?"

    Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, "Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari."

    16 Ndipo Pilato akamkabidhi Isa kwao ili wamsulubishe.

    Kwa hiyo askari wakamchukua Isa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    12 Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, "Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu yeyote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari."

    13 Pilato aliposikia maneno haya akamtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe, kwa Kiebrania paliitwa Gabatha19:13 Gabatha ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni Sakafu ya jiwe; ni mahali pa wazi palipoinuliwa ambako palitumika kama mahakama. 14 Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi.

    Pilato akawaambia Wayahudi, "Huyu hapa mfalme wenu!"

    15 Wao wakapiga kelele, "Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!"

    Pilato akawauliza, "Je, nimsulubishe mfalme wenu?"

    Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, "Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari."

    16 Ndipo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili wamsulubishe.

    Kwa hiyo askari wakamchukua Yesu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.