12 Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Isa, lakini viongozi wa Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, "Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu yeyote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari."
13 Pilato aliposikia maneno haya, akamtoa Isa nje tena. Akaketi kwenye kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe (kwa Kiebrania ni Gabatha). 14 Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi.
Pilato akawaambia Wayahudi, "Huyu hapa mfalme wenu!"
15 Wao wakapiga kelele, "Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!"
Pilato akawauliza, "Je, nimsulubishe mfalme wenu?"
Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, "Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari."
16 Ndipo Pilato akamkabidhi Isa kwao ili wamsulubishe.
Isa asulubishwa
(Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Luka 23:26-43)
Kwa hiyo askari wakamchukua Isa.