Pular para o conteúdo
Publicidade

João 4

Yesu amponya mwana wa ofisa

46 Yn 2:1-11Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na ofisa mmoja ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. 47 Lk 7:2Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yudea mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa karibu kufa. 48 Yn 2:18;1 Kor 1:22Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? 49 Yule ofisa akamwambia, Bwana, ushuke mtoto wangu asije akafa. 50 Yesu akamwambia, Nenda; mwanao yu hai. Mtu yule akaliamini lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia. 51 Mt 8:6Na alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. 52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa na nafuu; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha. 53 Lk 19:9;Mdo 16:15,31Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake. 54 Yn 2:11,23Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Yudea kwenda Galilaya.

Veja também