Publicidade

Jó 25

Bildadi anena: Mtu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu

1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,

2 Enzi na hofu zi pamoja na Mungu;

Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.

3 Je! Majeshi yake yahesabika?

Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?

4 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?

Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?

5 Tazama, hata mwezi hauangazi,

Wala nyota si safi machoni pake;

6 Seuze mtu, aliye mdudu!

Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-19_11-20-24-