Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 33

Elihu amkemea Ayubu

1 Ayu 13:6 Lakini, Ayubu, nakuomba usikilize hoja yangu,

Ukayasikilize maneno yangu yote.

2 Tazama basi, nimefunua kinywa changu,

Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.

3 1 The 1:3 Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;

Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.

4 Mwa 2:7 Roho ya Mungu imeniumba,

Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.

5 Ikiwa unaweza, nijibu;

Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.

6 Ayu 9:32 Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;

Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.

7 Ayu 13:21 Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,

Wala sitakulemea kwa uzito.

8 Hakika umenena masikioni mwangu,

Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,

9 Ayu 10:7 Mimi ni safi, sina makosa;

Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;

10 Ayu 13:24 Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami,

Hunihesabu kuwa ni adui yake;

11 Ayu 13:27 Hunitia miguu yangu katika mkatale,

Na mapito yangu yote huyapeleleza.

12 Mhu 7:20 Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki;

Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.

13 Isa 45:9 Kwa nini unapingana naye, ukisema,

Hatajibu hata neno langu moja?

14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,

Naam, hata mara ya pili, ijapokuwa mtu hatambui.

15 Ayu 4:13 Katika ndoto, katika maono ya usiku,

Usingizi mzito uwajiapo watu,

Katika usingizi kitandani;

16 Ndipo huyafunua masikio ya watu,

Na kuyatia mhuri mafundisho yao,

17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,

Na kumfichia mtu kiburi;

18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,

Na uhai wake usiangamie kwa upanga.

19 Kum 8:5;Zab 94:12,13 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,

Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;

20 Hata roho yake huchukia chakula,

Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.

21 Zab 102:5 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;

Na mifupa yake isiyoonekana yatokeza nje.

22 Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,

Na uhai wake unakaribia waangamizi.

23 2 Nya 36:15,16;Mal 2:7 Lakini akiwapo malaika pamoja naye,

Mpatanishi, mmoja katika elfu,

Ili kumwonesha binadamu hayo yampasayo;

24 Rum 3:24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,

Mwokoe asishuke shimoni;

Mimi nimeuona ukombozi.

25 Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;

Huzirudia siku za ujana wake;

26 2 Fal 20:2-5;Zab 6:1-9 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;

Hata auone uso wake kwa furaha;

Naye humrejeshea mtu haki yake.

27 Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,

Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,

Wala sikulipizwa jambo hilo;

28 Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni,

Na uhai wangu utautazama mwanga.

29 Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya,

Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,

30 Zab 40:2;Zek 9:11 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni,

Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.

31 Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize;

Nyamaza, mimi nitasema.

32 2 Kor 1:24 Kama una neno la kusema, nijibu;

Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.

33 Zab 34:11 Kama sivyo, unisikilize mimi;

Nyamaza, nami nitakufunza hekima.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também