Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 35

Elihu alaani haki ya ubinafsi

1 Tena Elihu akajibu na kusema,

2 Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako,

Au je! Wasema, Ni haki yangu mbele za Mungu,

3 Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe?

Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?

4 Mimi nitakujibu,

Na hawa wenzio pamoja nawe.

5 Ziangalie mbingu ukaone;

Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.

6 Ayu 22:2-3 Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake?

Ikiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?

7 Mit 9:12;Rum 11:35 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani?

Au yeye hupokea nini mkononi mwako?

8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe;

Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.

9 Kut 2:23;Neh 5:5;Ayu 24:12;Zab 12:5;Lk 18:3-7 Kwa sababu ya wingi wa dhuluma wao hulia;

Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.

10 Mhu 12:1;Isa 51:13;1 Pet 4:19;Zab 42:8;Mdo 16:25 Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu,

Awapaye nyimbo wakati wa usiku;

11 Ayu 32:8;Zab 8:6;1 Yoh 5:20 Atufundishaye zaidi ya wanyama wa nchi,

Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?

12 Mit 1:28 Hulia huko, lakini hapana ajibuye,

Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

13 Hakika Mungu hatasikia ubatili,

Wala Mwenyezi hatauangalia.

14 Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii,

Hiyo kesi i mbele yake, nawe wamngojea!

15 Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujia katika hasira zake,

Wala hauzingatii sana makosa;

16 Ayu 34:35,37 Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili;

Huongeza maneno pasipo maarifa.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também