Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 16

Ayubu asisitiza kuwa hana hatia

1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2 Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo;

Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.

3 Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho?

Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?

4 2 Fal 19:21;Zab 22:7;Yer 18:16;Omb 2:15 Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi;

Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu,

Ningeweza kutunga maneno juu yenu,

Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.

5 Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu,

Na maliwazo ya midomo yangu yangewatuliza.

6 Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi;

Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?

7 Lakini sasa amenichokesha;

Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.

8 Umenishika sana, na kuwa ushahidi juu yangu;

Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.

9 Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea;

Amesagasaga meno juu yangu;

Mtesi wangu hunikazia macho makali.

10 Zab 22:13;1 Fal 22:24;Omb 3:30;Mik 5:1;Mt 26:67;Yn 18:22;Mdo 23:2;Zab 35:15 Wamenifumbulia vinywa vyao;

Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;

Hukutana pamoja juu yangu.

11 Mungu amenitia kwa hao wapotovu,

Na kunitupa mikononi mwao waovu.

12 Nilikuwa katika raha, naye akanivunjavunja;

Naam, amenishika shingo, na kuniponda;

Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.

13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote,

Hunipasua figo zangu, asinihurumie;

Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.

14 Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu;

Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.

15 Zab 7:5 Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu,

Na nguvu zangu nimezibwaga mavumbini.

16 Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi,

Na giza tupu liko katika kope zangu;

17 Ijapokuwa hakuna udhalimu mikononi mwangu,

Na kuomba kwangu ni safi.

18 Ayu 27:9 Ee nchi, usiifunike damu yangu,

Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.

19 Ayu 19:25;Rum 1:9 Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni.

Na huyo atakayenidhamini yuko juu.

20 Rafiki zangu hunidharau;

Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;

21 Ayu 31:35 Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu,

Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.

22 Mhu 12:5 Kwani ikiisha pita miaka michache,

Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também