12 Kum 4:19;17:3;Zab 19:4;Isa 28:21;38:8;Hab 3:11;Amu 12:12Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli,
Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni;
Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
13 2 Sam 1:18Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia,
Hadi hilo taifa lilipokuwa limekwisha jilipiza kisasi juu ya adui zao.
Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima. 14 Isa 38:8;Kut 14:14;Kum 1:30;3:22;20:4;33:26-29;Yos 23:3,10;Amu 1:19,22;2 Nya 20:29;Neh 4:20;Zab 33:8-20;Isa 31:4;42:13;Zek 14:3Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizofuata baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.