12 Siku ile Mwenyezi Mungu alipowakabidhi Waamori kwa Waisraeli, Yoshua akanena na Mwenyezi Mungu akiwa mbele ya Waisraeli, akasema:
"Wewe jua, simama juu ya Gibeoni,
wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni."
13 Hivyo jua likasimama,
nao mwezi ukatulia,
hadi taifa hilo lilipokwisha
kujilipizia kisasi kwa adui zake,
kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari.
Jua likasimama katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku nzima. 14 Hakujakuwa na siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo Mwenyezi Mungu alimsikiliza mwanadamu. Hakika Mwenyezi Mungu alikuwa akiwapigania Israeli.