Ndoa ya Samsoni
1 Mwa 38:13;Yos 15:10;Mwa 34:2;Zab 119:37Samsoni akateremka hadi Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. 2 Mwa 21:21;34:4Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemuona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mniruhusu, nimuoe. 3 Mwa 24:3,4;Kut 34:16;Kum 7:3Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu wote, hata uende kumuoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mniruhusu nimuoe huyo, kwa maana ananipendeza sana. 4 Yos 11:20;2 Nya 10:15Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la BWANA; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.