Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 14:1-4

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Ndoa ya Samsoni

1 Samsoni akateremka Timna, na huko akamwona mwanamke Mfilisti. 2 Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, "Nimemwona mwanamke Mfilisti huko Timna; basi mnitwalie awe mke wangu."

3 Baba yake na mama yake wakamjibu, "Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa watu wetu wote, hata ulazimike kwenda kujitwalia mke kutoka kwa hao Wafilisti wasiotahiriwa?"

Lakini Samsoni akamwambia baba yake, "Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza." 4 (Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.)

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mwa 38:13;Yos 15:10;Mwa 34:2;Zab 119:37Samsoni akateremka hadi Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. 2 Mwa 21:21;34:4Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemuona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mniruhusu, nimuoe. 3 Mwa 24:3,4;Kut 34:16;Kum 7:3Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu wote, hata uende kumuoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mniruhusu nimuoe huyo, kwa maana ananipendeza sana. 4 Yos 11:20;2 Nya 10:15Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la BWANA; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Samsoni akateremkia Timna, akamwona mwanamke wa Kifilisti. 2 Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, "Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipe ili awe mke wangu."

    3 Baba yake na mama yake wakamjibu, "Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda kujitwalia mwanamke kutoka kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa?"

    Lakini Samsoni akamwambia baba yake, "Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza." 4 (Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa Bwana, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.)

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.