4 Wim 2:15;Eze 13:4Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa mienge ya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia mwenge kati ya kila mikia miwili. 5 Alipokwisha kuiwasha moto ile mienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti, akayateketeza matita, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni. 6 Amu 14:15Ndipo Wafilisti wakasema, Ni nani aliyetenda hivi? Wakasema, Ni huyo Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake. Wafilisti wakaenda wakamteketeza yeye na baba yake kwa moto.
14 Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. 15 Law 26:8;Kum 32:30;Yos 23:10;Amu 3:31;1 Sam 14:6,12-16;2 Sam 23:8Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akaua watu elfu moja kwa mfupa huo;
20 Amu 13:1Naye akawa mwamuzi wa Israeli: katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini.