Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 15:4-6,14,15,20

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

4 Hivyo Samsoni akaondoka na kuwakamata mbweha mia tatu, akawafunga wawili wawili, mikia kwa mikia. Kisha akafungia mwenge wa moto kwenye kila jozi la mikia hiyo. 5 Akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka, pamoja na mashamba ya mizabibu na mashamba ya mizeituni.

6 Wafilisti walipouliza, "Ni nani aliyetenda jambo hili?" Wakaambiwa, "Ni Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu mkewe alipeanwa kwa rafiki yake."

Hivyo Wafilisti wakapanda, wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake.

14 Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 15 Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao elfu moja.

20 Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    4 Wim 2:15;Eze 13:4Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa mienge ya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia mwenge kati ya kila mikia miwili. 5 Alipokwisha kuiwasha moto ile mienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti, akayateketeza matita, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni. 6 Amu 14:15Ndipo Wafilisti wakasema, Ni nani aliyetenda hivi? Wakasema, Ni huyo Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake. Wafilisti wakaenda wakamteketeza yeye na baba yake kwa moto.

    14 Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. 15 Law 26:8;Kum 32:30;Yos 23:10;Amu 3:31;1 Sam 14:6,12-16;2 Sam 23:8Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akaua watu elfu moja kwa mfupa huo;

    20 Amu 13:1Naye akawa mwamuzi wa Israeli: katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    4 Hivyo Samsoni akatoka akawakamata mbweha 300 na kuwafunga wawili wawili kwa mikia yao kila mmoja kwa mwingine. Kisha akafungia mwenge wa moto, kwenye mikia ya kila jozi moja ya mbweha aliyokuwa ameifunga, 5 akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka zilizosimama, pamoja na mashamba ya mizabibu na viunga vya mizeituni.

    6 Ndipo Wafilisti wakauliza, "Ni nani aliyetenda jambo hili?" Wakaambiwa, "Ni Samsoni, yule mkwewe Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake."

    Hivyo Wafilisti wakapanda wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake.

    14 Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 15 Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao 1,000.

    20 Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.