Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 16:1-3

SRUV Swahili Revised Union Version

Samsoni na Delila

1 Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. 2 1 Sam 19:11;23:26;Zab 118:10-12;Mdo 9:24;2 Kor 11:32,33Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua. 3 Basi Samsoni akalala hadi usiku wa manane, akaamka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hadi katika kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, "Samsoni amekuja huku!" Hivyo, wakapazingira mahali pale, nao wakamvizia usiku kucha penye lango la mji. Wakakaa kimya usiku kucha, wakiwaza, "Kutakapopambazuka, tutamuua."

    3 Samsoni akalala tu hadi usiku wa manane. Akaamka, na kushika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na makomeo yake. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka hadi kilele cha mlima unaokabili Hebroni.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, "Samsoni amekuja huku!" Hivyo wakapazingira mahali pale nao wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji. Wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, "Tumvizie hadi mapambazuko, ndipo tutamuua."

    3 Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati ya usiku, akashika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaingʼoa, makomeo yake na vyote. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka mpaka kwenye kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.