Samsoni na Delila
1 Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, "Samsoni amekuja huku!" Hivyo, wakapazingira mahali pale, nao wakamvizia usiku kucha penye lango la mji. Wakakaa kimya usiku kucha, wakiwaza, "Kutakapopambazuka, tutamuua."
3 Samsoni akalala tu hadi usiku wa manane. Akaamka, na kushika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na makomeo yake. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka hadi kilele cha mlima unaokabili Hebroni.