Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 16:18-22

SRUV Swahili Revised Union Version

18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia siri yake yote. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. 19 Mit 5:3,4;7:21;Mhu 7:25,26Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. 20 Hes 14:9,42,43;Yos 7:12;1 Sam 16:14;18:12;28:15,16;2 Nya 15:2;Zab 33:16;Mit 22:14;Yer 9:23,24;Hos 9:12Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha. 21 Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza. 22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    18 Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, "Njooni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote." Basi viongozi wa Wafilisti wakarudi kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao. 19 Delila akamfanya alale usingizi magotini pake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake. Delila akaanza kumnyong’onyesha Samsoni, nazo nguvu zake zikamtoka.

    20 Yule mwanamke akamwita, "Samsoni! Hao, Wafilisti wanakujia!"

    Akaamka toka usingizini, akisema, "Nitatoka nje kama hapo awali; nitajinyoosha, niwe huru." Lakini hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemwacha.

    21 Basi Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho yake, wakamteremsha hadi Gaza. Wakamfunga kwa pingu za shaba, wakamweka gerezani ili asage ngano. 22 Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    18 Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, "Njooni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote." Basi viongozi wa Wafilisti wakaja kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao. 19 Delila akamfanya alale usingizi magotini pake, akamwita mtu akamnyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake. Akaanza kumsumbua ili aamke nazo nguvu zake zikamtoka.

    20 Yule mwanamke akamwita, "Samsoni, hao Wafilisti wanakujia!"

    Akaamka toka usingizini akasema, "Nitatoka nje kama hapo awali, nitawakungʼutia mbali na kuwa huru." Lakini hakujua kuwa Bwana amemwacha.

    21 Basi Wafilisti wakamkamata, wakamngʼoa macho yake, wakamchukua wakamteremsha mpaka Gaza. Wakiwa wamemfunga kwa pingu za shaba, wakamweka ili asage ngano huko gerezani. 22 Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.