18 Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, "Njooni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote." Basi viongozi wa Wafilisti wakarudi kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao. 19 Delila akamfanya alale usingizi magotini pake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake. Delila akaanza kumnyong’onyesha Samsoni, nazo nguvu zake zikamtoka.
20 Yule mwanamke akamwita, "Samsoni! Hao, Wafilisti wanakujia!"
Akaamka toka usingizini, akisema, "Nitatoka nje kama hapo awali; nitajinyoosha, niwe huru." Lakini hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemwacha.
21 Basi Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho yake, wakamteremsha hadi Gaza. Wakamfunga kwa pingu za shaba, wakamweka gerezani ili asage ngano. 22 Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa.