Ehudi
12 Amu 2:19;Yer 16:12;Hos 6:4;Mt 23:32;1 Sam 12:9Basi wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za BWANA; naye BWANA akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA. 13 Amu 5:14;Kum 34:3;Amu 1:16Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende.