Ehudi
12 Amu 2:19;Yer 16:12;Hos 6:4;Mt 23:32;1 Sam 12:9Basi wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za BWANA; naye BWANA akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA. 13 Amu 5:14;Kum 34:3;Amu 1:16Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende. 14 Law 26:23-25;Kum 28:40Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane. 15 Zab 50:15;78:34;Yer 29:12,13;Dan 9:3;Amu 20:16Lakini wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi. 16 Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kulia. 17 Kisha akamsogezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyenenepa sana. 18 Naye hapo alipomaliza kuitoa hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. 19 Yos 4:20Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu naye wakatoka na kumwacha. 20 Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, "Nina ujumbe wako kutoka kwa Mungu". Basi akainuka katika kiti chake. 21 Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kulia, akamtia tumboni mwake; 22 hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma.3:22 Maana ya neno la Kiebrania si dhahiri.23 Ndipo Ehudi akatoka nje barazani,3:23 Maana yake katika Kiebrania si dhahiri. akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo. 24 Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi ameenda haja3:24 Katika Kiebrania ni kufunika miguu. ndani ya chumba cha baridi. 25 Wakangoja hadi wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka chini, naye amekufa. 26 Naye Ehudi alikimbia hapo walipokuwa wakingoja, Ehudi alitoroka kwa kupitia huko kwenye sanamu, na kukimbilia Seira. 27 Amu 5:14;6:34;1 Sam 13:3;Yos 17:15;Amu 7:24;17:1Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia. 28 Amu 7:9,15;1 Sam 17:47;Yos 2:7;Amu 12:5Akawaambia, Nifuateni; kwa kuwa BWANA amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakateremka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka. 29 Wakati huo wakawaua Wamoabi wapatao wanaume elfu kumi, ambao wote walikuwa wenye nguvu na mashujaa, hakunusurika hata mtu mmoja. 30 Basi Moabu alishindwa siku hiyo chini ya mikono ya Israeli. Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka themanini.