Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 1

Wimbo wa Sifa wa Mariamu

46 1 Sam 2:1-10Mariamu akasema,

Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

48 1 Sam 1:11;Lk 1:25;Zab 113:5,6;Lk 11:27Kwa kuwa ameutazama

Unyonge wa mjakazi wake.

Kwa maana, tazama, tokea sasa

Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

49 Zab 111:9Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,

Na jina lake ni takatifu.

50 Zab 103:13,17Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi

Kwa hao wanaomcha.

51 Zab 89:10;2 Sam 22:28Amefanya nguvu kwa mkono wake;

Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52 Ayu 5:11;12:19;Zab 147:6;1 Sam 2:7Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;

Na wanyonge amewainua.

53 1 Sam 2:5;Zab 34:10;107:9Wenye njaa amewashibisha mema,

Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

54 Isa 41:8;Zab 98:3Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;

Ili kukumbuka rehema zake;

55 Mwa 17:7;18:18;22:17;Mik 7:20Kama alivyowaambia baba zetu,

Abrahamu na uzao wake hata milele.

Veja também