59 Law 12:3;Mwa 17:12Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. 60 Lk 1:13Mamaye akajibu akasema La, sivyo; bali, ataitwa Yohana. 61 Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo. 62 Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita. 63 Akataka kibao, akaandika ya kwamba, Jina lake ni Yohana. Wakastaajabu wote.