Yesu aulilia Yerusalemu
41 2 Fal 8:11;Yn 11:35Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 Kum 32:29;Mt 13:14;Yn 12:38akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 Lk 21:6;Zab 137:9watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiwa kwako.