Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 19:41-44

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Isa aulilia mji wa Yerusalemu

41 Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, 42 akisema, "Laiti ungejua, hata wewe leo, yale yangeleta amani, lakini sasa yamefichika machoni pako. 43 Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. 44 Watakuponda chini, wewe na watoto walio ndani ya kuta zako. Nao hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukutambua wakati wa kujiliwa kwako."

Isa atakasa Hekalu

(Mathayo 21:12-17; Marko 11:15-19; Yohana 2:13-22)

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    41 2 Fal 8:11;Yn 11:35Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 Kum 32:29;Mt 13:14;Yn 12:38akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 Lk 21:6;Zab 137:9watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiwa kwako.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    41 Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, 42 akisema, "Laiti ungalijua hata wewe leo yale ambayo yangeleta amani, lakini sasa yamefichika machoni pako. 43 Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. 44 Watakuponda chini, wewe na watoto walioko ndani ya kuta zako. Nao hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukutambua wakati wa kujiliwa kwako."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.