Sadaka ya mjane
1 Mk 12:41-44Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. 2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. 3 2 Kor 8:12Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; 4 maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.