Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 21:1-4

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Sadaka ya mjane maskini

1 Isa alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. 2 Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba. 3 Isa akasema, "Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote. 4 Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali yao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi."

Kubomolewa kwa Hekalu kwatabiriwa

(Mathayo 24:1-2; Marko 13:1-2)

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mk 12:41-44Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. 2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. 3 2 Kor 8:12Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; 4 maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. 2 Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba. 3 Yesu akasema, "Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote. 4 Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.