Kuja kwa Mwana wa Adamu
25 Mt 24:29,30;Mk 13:24-26Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa kuvuma kwa habari na mawimbi yake; Isa 13:10;Eze 32:7;Yoe 2:31;Ufu 6:12-13;Zab 65:726 Isa 34:4watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.