Maandalizi ya Pasaka
7 Mt 26:17-29;Mk 14:12-25Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja Pasaka. Kut 12:18-208 Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie Pasaka tupate kuila.
Kuanzishwa kwa chakula cha Bwana
14 Na saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 19 1 Kor 11:23-25;Mdo 27:35Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20 Kut 24:8;Yer 31:31;Zek 9:11Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]