7 Basi ikawadia siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa. 8 Hivyo Isa akawatuma Petro na Yohana, akisema, "Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuweze kuila."
14 Wakati ulipowadia, Isa akaketi mezani pamoja na wale mitume wake. 15 Kisha akawaambia, "Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.
19 Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, "Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu."
20 Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu.