Mwanamke mwenye dhambi asamehewa
36 Lk 11:37Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37 Mt 26:7-13;Mk 14:3;Yn 12:3-8Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. 38 Mt 26:7-13;Yn 12:3-8Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusubusu miguu yake na kuipaka yale marhamu. 47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. 48 Lk 5:20,21Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako. 50 Lk 8:48;17:19;18:42Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, nenda zako kwa amani.