Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 9

Kutumwa kwa wale kumi na wawili

1 Mt 10:1,7,9-14;Mk 6:7-13Akawaita wale Kumi na Wawili, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. 2 Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kuponya wagonjwa. 3 Lk 10:4-11;Mdo 13:51Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. 4 Lk 10:5-7Na nyumba yoyote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini. 5 Lk 10:11Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung’uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao. 6 Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri Injili, na kuponya watu magonjwa kila mahali.

Veja também