Pular para o conteúdo
Publicidade

Levítico 21

Utakatifu wa makuhani

1 Law 5:2;Eze 44:25 Kisha BWANA akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake; 2 isipokuwa ni kwa ajili ya jamaa yake wa karibu, kwa ajili ya mama yake, na kwa ajili baba yake, na kwa ajili ya mwanawe, na kwa ajili ya binti yake, na kwa ajili ya nduguye mwanamume; 3 na kwa ajili ya dada yake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mwanamume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo. 4 Asijitie unajisi, ijapokuwa ni mkubwa katika watu wake, hata akajinajisi. 5 Law 19:27-28;Kum 14:1;Eze 44:20 Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje tojo katika miili yao. 6 Kut 20:7;Law 18:21;19:12;Kum 5:11;Zab 15:4;Mt 5:33-37;Yak 5:12;Law 3:11 Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu. 7 Eze 44:22;Kum 24:1,2 Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake. 8 Law 20:7,8;Isa 43:15 Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi BWANA niwatakasaye ninyi ni mtakatifu. 9 Mwa 38:24 Na binti ya kuhani yeyote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa hadi afe.

10 Kut 29:29;Hes 35:25;Kut 28:2;Law 10:6 Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake; 11 Hes 19:14 wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake; 12 Law 10:7;Kut 28:36;Law 8:9,12,30 wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake uko juu yake; mimi ndimi BWANA. 13 Eze 44:22 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. 14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe. 15 Rum 12:1;1 Kor 3:16,17;Efe 5:17;1 The 4:1-8 Naye asiwatie unajisi wazawa wake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.

16 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 17 Hes 16:5;Zab 64:4 Nena na Haruni, umwambie, Mtu yeyote wa vizazi vyenu vyote aliye na kilema asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake. 18 Law 22:23 Kwa kuwa mtu aliye na kasoro ya kimwili hatakaribia, asiyeoana, aliyelemaa mguu au mtu aliyejeruhika uso, au kiungo kilichozidi vimpasavyo mwili, 19 au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono, 20 Kum 23:1 au aliye na kibyongo, au aliyedumaa, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu; 21 mtu yeyote wa wazawa wa Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. 22 Law 2:3,10;22:10;Hes 18:19 Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu. 23 Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye. 24 Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.

Veja também