25 Rut 2:20;3:2Ikiwa nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye.
47 Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; 48 baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa; 49 au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu yeyote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kama yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe.